Preloader

Watawa wa SCIM miaka 75. Ni yubilei!

"Bikira Maria ananiangaza nianzishe Shirika la watawa wa kiume" yaani “mabruda”. Ndivyo alivyokuwa akisema Mons. Attilio Beltramino, mmisionari wa Consolata, mwanzilishi wa Shirika la Watumishi wa moyo safi wa Bikira Maria, kwa lugha ya kilatini, Servi Cordis Immaculati Mariae (SCIM). Ni Shirika la kijimbo lililoanzishwa na askofu huyu wa kwanza wa Jimbo la Iringa, nchini Tanzania mnamo tarehe 31 Mei 1949. Ni miaka 75 imepita tangu wakati huo. Wapendwa ni shangwe, ni yubilei!
Tarehe 8 Juni 2024, sikukuu ya Moyo Mtakatifu wa Maria, ilifanyika jubilei hiyo Tosamaganga, mahali ilipo pia nyumba mama ya Shirika. Siku hiyo ilishuhudia watu wengi kutoka sehemu mbalimbali za Tanzania wakikusanyika kumshukuru Mungu kwa mambo makuu ambayo Bwana ametenda katika miaka hii 75. Waliohudhuria ni pamoja na askofu wa Iringa Mons. Tarcisius Ngalalekumtwa, Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania na askofu mkuu wa jimbo kuu la Mbeya Mons. Gervas Nyaisonga, Balozi wa Baba Mtakatifu Tanzania Mons.