About Consolata Centenary School
Ni shule ya secondary inayosimamiwa na wamisionari wa consolata. Shule hii ni matunda ya Jublei ya miaka mia moja ya uinjilishaji nchini Tanzania. Shirika la wamisionari wa Consolata linalenga katika kumsaidia mwanadamu kiroho na kimwili. Hivyo basi Wamisionari wa Consolata Consolata wanaungana na serikali ya Tanzania katika kutoa elimu ya sekondari na elimu amali. Shule hii imepanga kutumia Chuo cha veta na workshop zake kuhakikisha kwamba mwanafunzi anapomaliza elimu yake ya sekondari pia amebobea katika fani aliyoichagua.
Shule inayo vitendea kazi vya kutosha kwa ajili ya wanafunzi wote, na pia wapo waalimu waliobobea katika kufundisha masomo ya kawaida na ufundi ili kujenga uwezo wa mwanafunzi kujitegemea.
