About St. Joseph Parish - Sanza
UINIJILISHAJI KUANZIA WAMISIONARI WA KWANZA 1947-1951
1. Kutoka Bihawana walifika Mapadre ambao ndio waanzilishi wa kuleta Uinjilishaji (utume) dini ya Ukatoliki huko (Chinoje) Ikassi. Nao ni Padre ADOLFU na mwenzake JULIAN BELLAVIT. Na walijenga nyumba ndogo ya kufikia pale Chinoje. Hivyo walianza mara moja kazi ya uinjlishaji kwa kutafuta waumini. Walikuwa wanafanya kazi hiyo kwa siku kadhaa na kurudi tena Bihawana.
2. Mapadre hawa walikuwa wanatoka jimbbo katoliki la Dodoma. Na Askofu wa jimbo kwa wakati huo alikuwa ni Mhashabu Baba Askofu Jerrremia Pesce, na paroko wa parokia ya Bihawana alikuwani padre Yohani; wote walikuwa ni mapadre wa shrika la mateso (passionist fathers) kutoka Dodoma.
3. Mapadre hawa Pd. ADOLFU na Pd. JULIAN BELLAVITI, Waliinjilisha na kuoata waumini katika vijiji vifuatavyo; Ikassi, Chali Isanga, Igongo, Chipanga, Ntumbi, Isseke, Igwamadete, Mpapa, Simbanguru, Mahangalenga, Sanza, Nkonko, Makopa, Chitunja, Zenjele, Chifutuka, Magaga, Chitwechambwa, Ilangari, Makasuku, Majiri, Nondwa na Chikopelo. Kazi hiyo ya uinjilishajina kutafuta waumini walitumia usafiri wa baiskeli na baadae pikipiki ndogo aina ya Honda.
4. Baada ya hapo Mapadre hao walishindwa kuendeleza kituo cha Chinoje (Roki) hapo Ikassi kutokana na changamoto zifuatazo
a) Wakati huo ulikuwa ni utawala wa watemi waliokuwa wamewekwa na wakoloni wa Waingereza. Hapo Ikassi alikuwepo mtemi aliyekuwa naitwa Bodyo Maloda. Hawa watemi hawakupenda kupokea wageniwa Kizungu au Waarabu kukaa katika vijiji vyao. Walijihisi kuwa watanyang’anywa utawala wao.
b) Tatizo la upatikanaji wa maji hapo Chinoje (Roki)- Ikassi ilikuwa shida sana.
5. Kutokana na changamoto hizo, mwaka 1948 walianzisha makazi mapya sehemu iliko zahanati ya Mission Sanza. Hapo katika eneo la zahanati ya Mission Sanza palikwana mti uitwao Mduguyu kwa lugha ya Kigogo. Katika eneo eneo hilo walijenga hema la kulala Mapadre. Pia walijenga kikanisa kidogo cha vyumba viwili vilivyotumika kama stoo na darasa kwa ajili ya kufanyia ibadana mafundisho ya wakatukumeni. Mwaka 1949 wakiwa katika ujenzi wa Mission hapa Sanza parokiani, alifika Askofu wa Jimbo la Dodoma Mhashamu Askofu Jeremia Pesce kuangalia ujenzi unavyoendelea aliwatia moyo na nguvu ili waendelee na ujenzi huo.
6. Mwaka 1950 Mapadre hawa walihaishwana mwaka huo huo 1950 waliletwa padre Plasido Tonneli akawa paroko wa kwanza akisaidiwa na Pd. Tito Beduchi, Pd. Marino Zambon na Pd. Masweto na Bruda Cassiano na baadae Bruda Bernado. Hivyo Mapadre waliendelea na uinjilishaji wa kutafuta waumini katika vijiji mbalimbali na ujenzi wa majengombalimbali hapa Mission.
7. Parokia ya Sanza wakati huo ikiongozwa na aliyekuwa paroko padre Plasido Tonneli akisaidiana na wenzake waliotajwa hapo juu ikawa imefunguliwa rasmi. Hivyo wamisionari hawa waliendela kufanya utume pamoja hadi mwaka 1966, ambapo Padre Plasido Tonneli alienda likizo ulaya na nafasi yake ya uparoko akapewa Padre Marino Zambon.
Padre Marino Zambon paroko mwaka 1966 alijenga kanisa la parokia ambao lilo lipo mpaka sasa (2023). Lilikuepo kanisa dogo lililokuwa linatumika hapo awali kama kanisa na darasa, mahali ilipo nyumba ya Mapadre pamoja na jengo la kanisa lilikuwa ni eneo la shamba la mwenyeji mmoja aliyeitwa MNYAGUNGU MNYAUSI, Aliyeitwa VALAKU MOMELWA. Eneo hilo lilinunuliwakwaTsh 30/= (Thelethini). Fedha hiyo alikabidhiwamzee MHAHA MAGOBOO Mjukuuwa VALAKU.
Pamoja na juhudi za uinjilishaji Wamissionari hawa walikumbana na matatizo mbalimbali na Mtawala wa wakati huo Mtawala alikwa Mtemi KAPANDE NTAWA wa kijiji cha Sanza. Changamoto nyingine ilitokea mwaka 1958 wanakijiji walileta vurugu kubwa walifanya Mapadre wote kuhama na kurudi Bihawana; kwa mwaka mzima kwa kutambua umuhimu wa utume wao mwaka uliofuata (1959)walirudi tena parokiani Sanza kuendelea na ujenzi wa Mission na uinjilishaji.
8. Mapadre wa kwanza waliofika Chinoje (Roki) - Ikassi na baadae Sanza walifanya kazi chini ya parokia ya Bihawana. Hivyo hkuna kumbukumbuku muhimu za waumini za waumini wa mwanzo kwa mfano wabatizwa wa wakati ule, zilibaki parokia ya Bihawana, hivyo hakuna kumbukumbu sahihi za paokia ya Sanza ilivyoanza.
HUDUMA MBALIMBALI ZILIZOFANYIKA NA PADRE PLASIDO NA WENZAKE KUANZIA MWAKA 1950- 1963
I. Kujenga jingo kubwa la kuishi Mapadre lenye ghoroa moja na ndilo wanaishi Mapadre mpaka sasa.
II. Kuanzisha shamba kubwa kwa ajili ya kilimo na kuweka mipaka eneo lote la hapa parokiani kwa kuchimbia minyaa kwa sasa minyaa hiyo imekufa.
III. Kuchimba kisima cha maji na kuanzisha bustani kubwa iliyopandwa maembe, mapapai, mapera, mafenesi, machungwa, marimau, mizabibu na mbogamboga za kila ainapamojana maua. Kisima hicho kilijengwa kuanzia chini kwa matofari ya kuchomwa na maji yalivutwa kwa mashine ndogo na kusambazwa kwa mabomba kwa kutumia dizeli.
IV. Katika kazi ya ujenzi Padre Plasido na wenzake walileta kundi la vijana kutoka Mission ya Kulyo Usandawi kwajili ya kufyatua matofari ya kuchoma wakisaidiana na wananchi wa hapa Sanza. Kazi hizi walizifanya kwa kulipwa.
V. Walianzisha ufugaji wa ng’ombe, mbuzi, kondoo na bata. Pia palikuwepo zahanati ndogo ya Mission. jengo hilo lilijengwa ambalo jingo la Masista wanaishi sasa. Mganga wa zahanati alikuwa ni Pd. Tito Betuchina baadae aliletwa mganga aliyeitwa Sales
VI. Mwaka 1952 Mapadre hawa wa Shirika la Mateso walikusanya viana wengi wa kiume kutoka vijiji mbalimbali na waliwajengea mabweni (vyumba) wakawa wanaishi hapa hapa. Lengo kuu ni kwa ajili ya kusoma shule ya msingi na dini kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la nne (1-4). Ada walikuwa wanalipa wazazi wao lakini hapa wanaishi bure. Vijana hawa walikuwa wanalima shamba kwa ajili ya chakula chao. Mpango huo uliendelea mpaka 1966 ukawa umefungwa.
SHULE ZILIZOJENGWA NA WAMISIONARI HAWA KUANZIA DARASA LA 1 HADI 4
a) Shule Ya Sanza Ilijengwa Na Kufunguliwa Mwaka 1952
b) Shule Ya Chali Isanga, Ikassi, Nondwa Na Mpapa
c) Masista Wa Mwanzo Waliletwa Na Pd. Plasido Mwaka 1961- 1979. Walikuwa Ni Masistawa Mt. Gemma Galgani –Dodoma. Mama Mkubwa Wao Wa Nyumba Likuwa Ni Hayati Sista Gemma Ichuka Aliyekuwa Mmoja Wanashirika Wa Kwanza. Jumla walikuwa watano (5). Mmojawapo alikuwa mwalimu wa shule ya msingi Sanza aliyeitwa JANE FRANCHESCA
d) Walimu waliokuwawanafundisha shule ya msingi kwa wakati ule walikuwa wanaletwa kutoka Vyuo vya Ualimu Vilivyokuwa vinamilikiwa na Kanisa Katoliki. Kutoka kwa Askofu Jeremia Pesce wanafunzi waliofaulu walipelekwa BIHAWANA MIDDLE SCHOOL na KIGWE MIDDLE SCHOOL.
Parokia hii ya Mt. Yoseph Baba Mlishi wa Yesu Kristu Sanza hadi sasa ina vigango vyenye makanisa ya kudumu yaliyojengwa na Mapadre wa Shirika la Bikira Maria Consolata. Vigango hivyo ni kama vifuatavyo; Ikassi, Ntope, Igwamadete, Isseke, Nkonko, Mpola, Ntumbi, Mpapa, Simbanguru, Mangoli, Iwumba, Maona, Chihundiche na Chidudu.
Na idadi ya waamini inaendelea kuongezeka pamoja na vyama vya kitume vilivyopo parokiani navyo ni WAWATA, VIWAWA, TYCS, SHIRIKA LA MT. ANNA, UMAKASI, UWAKA, UTOTO MTAKATIFU. Kuna vigango 18 na Makatekista 23 na Waseminari 3 na Waseminari wakubwa 2.
Awamu ya pili ya Masista wa Shirika la Mtakatifu Gemma Galgan walirudi mwaka1992 mpaka sasa. Kwasasa tuna Masista 3 wa Shirika hilo.
10. “A”:
KAZI ZA MAENDELEO PAMOJA NA MIRADI ILIYOFANYIKA NA KANISA KATOLIKI KUANZIA MWAKA 1952 HADI SASA
i. ELIMU; Shule za msingi zilizokuwa zinaendeshwa na kanisa Katoliki zilikabidhiwa kwa serikali mwaka 1967 baada ya Azimio la Arusha
ii. ELIMU YA AWALI; Kuna shule za awali kwa baadhi ya vigango. Shule hizi bado zinaendelea kama vile Ntope, Sanza, Iwumba, Igwamadete, Mpapa na Maona.
iii. SHULE YA KAZI; Kulikuwepo na shule ya kazi Sanza kigangoni kwa ajili ya vijana wanaume waliokuwa wanafundishwa uselemara, kilimo kwa kutumia ng’ombe, ufundi wa uashi na ufyatuaji wa tofari za kuchoma na vigae. Baadae shule ilifungwa mwaka 1988
iv. VISIMA VYA MAJI; Kuna visima vya maji ambavyo vilichimbwa na Mapadre wa Shirika la Consolata kwa baadhi ya vigango kama vile Igwamadete, Mpapa, Iwumba, Mangoli na Nkonko.
v. AFYA; Kuna zahanati ya Kanisa Katoliki Parokia ya Sanzainayotoa huduma mpaka sasa. Masista wa Mt Gemma Galgan ndiyo wanaotoa huduma hiyo.
vi. KILIMO; Kuna mashamba yanayotumika katika shughuli ya kilimo katika vigango………………………. Ambavyo vinalima mazao ya alizeti na mahindi mpaka sasa.
vii. UFUGAJI; Hapa parokiani kuna ufugaji wa ng;ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe kwa ajili ya huduma kwa Mapadre
viii. Kuna majengo ya waliokuwa wanaishi vikongwe; majengo mawili kwa sasa hayatumiki, yapo mtaa wa mchetye kigango cha Sanza.
ix. Kuna jingo moja lenye vyumba viwili, mtaa wa Chitinde - Sanza na vyumba vitatu huko Simbanguru.
x. Kuna mashine ya kukamulia alizeti ipo parokiani na inafanya kazi.
“B” HUDUMA ZA KIROHO KIPAROKIA
i. Vigango vyote vya parokia vina jumuiya ndogo ndogo za Kikristu hadi sasa
ii. Vigango vyote vya parokia vina Makatekista wanafanya kazi ya uinjilishaji
iii. Vigango vyote vina vyama vya kitume
iv. Vigango vyote vina uongozi wa H/Walei. Kuanzia ngazi ya jumuiya hadi parokia kuna uongozi
v. Waumini wanazidi kuongezeka mwaka hadi mwaka
