About St. Mark the Evangelist Parish - Mji Mwema
PAROKIA YA MT. MARCO-MJI MWEMA
Anuani: Catholic Church Mji Mwema PO BOX 36130 Kigamboni Dar es Salaam.
Parokia ya Mt. Marco Mji Mwema ilianzishwa tarehe 26/4/2013. Hii ni parokia ambayo ipo pembezoni mwa mji wa Dar es Salaam, ng’ambo ya bara Hindi. Paroko mwanzilishi ni hayati padre Angelo Parola Imc, akipokewa na padre Emanuel Chacha imc ambaye alikuwa paroko toka mwaka 2014 mpaka 2017. Sasa hivi wapo padre Marco Turra imc na padre Salvador Del Molino Imc.
Lengo la parokia hii ni huduma ya kichungaji kwa watu wanaoishi katika maeneo ya Mji Mwema, na vigango vyake 6, ambavyo ni Kibugumo, Gezaulole, Mwongozo, Malimbika, Mchikichini, Vumilia Ukooni. Tunapakana na parokia za kigamboni na Kimbiji, nazo ni parokia wanapofanya kazi wamisionari wa Consolata. Miradi wa kutegemeza parokia yetu ni kukodisha maduka (fremu) na Shule ya awali katika kigango cha Gezaulole.
