Preloader

About Consolata Parish - Kigamboni

HISTORIA YA PAROKIA YA BIKIRA MARIA CONSOLATA KIGAMBONI
Parokia ya Bikira Maria Consolata -Kigamboni ilianzishwa mwaka 1973 na wamisionari Waconsolata chini ya uongozi wa Padre ORSOLA ambaye alikuwa Paroko wa Kwanza, akisaidiwa na maparoko wasaidizi.
Tangu mwaka 1973 hadi leo, Parokia ya Bikira Maria Consolata imefanikiwa kuanzisha Parokia sita; ambazo ni: Kimbiji, Mjimwema, Kibada, Mikwambe, Vijibweni. Parokia ya Kigamboni inaundwa na Jumla ya Kanda nne ambazo ni: Kivukoni, Kisiwani, Tuamoyo na Tungi. Parokia ina jumla ya Jumuiya Ndogondogo za Kikristo 40 ambazo zimegawanywa katika kanda hizi nne kama ifuatavyo;
Kanda ya Kivukoni Jumuiya 9
Kanda ya Kisiwani Jumuiya 8
Kanda ya Tuamoyo Jumuiya 11
Kanda ya Tungi Jumuiya 12
Parokia pia ina vyama vya kitume kama ifuatavyo: UWAKA; WAWATA; VIWAWA, UTOTO MTAKATIFU, Mt Vicent wa Paulo, Karismatiki Katoliki, Lejio Maria, UKWAKATA, Moyo
Mtakatifu wa Yesu, Watumishi wa Altare, Focolare Movement, Walei Waamigoniani, Makatekista, Wasoma Masomo, Wazee Wastaafu. Parokia inaundwa na kamati mbalimbali kuanzia Kamati
Tendaji Parokia, Kanda, na Jumuiya Ndogondogo. Parokia ipo katika mazingira inazungukwa na Dini, Madhehebu mbalimbali na baadhi ya Taasisi mbalimbali za serikali na za kijamii.
Kwa sasa Parokia inahudumiwa na mapadre wa Shirika la Consolata.

MISSION GALLERY