About St. Joseph the Worker Parish - Mkundi
HISTORIA YA PAROKIA
Parokia yetu ilianza rasmi mnamo tarehe 09.10. 2021 kwa tangazo la Baba Askofu Lazarus Vitalis Msimbe. Kigango cha Mkundi kina historia ndefu Zaidi. Mkundi, parish Centre ni kigango cha zamani sana kabla ya uhuru. Kilihamia Kihonda baada ya operation songesa. Kigango cha sasa kilianza upya miaka ya 20 iliyopita na kimehudumiwa kwa miaka mingi na wamisionari wa Consolata wa nyumba ya malezi (novitiate) Makunganya, kikiwa ni kigango cha parokia ya Mtakatifu Monika Kihonda.
IDADI YA JUMUIYA, KANDA NA VIGANGO
Parokia yetu inakua kwa kasi ambako mpaka sasa kuna jumuiya zipatazo 96. Ni kweli kwamba jumuiya zingine ni ndogo sana na ushiriki pia ni hafifu. Katika kigango mama pekee (Mkundi) jumuiya na 47. Pamoja na kigango mama, parokia ina vigango viwili,Kiegea na Makunganya). Pia kuna kanda 8 zenye vituo vya sala, ambazo bado hazina hadhi ya vigango. Navyo ni: Mji Mpya, Ngongele, Bwawani, Mkambarani, Maili 18A, Maili 18B, Maji Chumvi na Njovu.
