Preloader

About Mary Mother of Grace Parish - Makambako

INSPIRATION
“… Doing with sacrifice and dedication, witnessing to God’s love with simplicity and closeness to people, continuing the tradition of so many confreres who have preceded us, is remarkable…” XIV GC NO. 65
1. UTANGULIZI
Missioanri wa Consolata wa kwanza kufika Makambako kwa ajili ya uinjilishaji au kazi ya kitume ni padre Alfredo Ponti aliyetumwa na Mwashamu Baba askofu Beltamino imc kutoka Tosamaganga kati ya Mwiaka 1948-1949…kumbe Mission ya Makambako ilianza rasmi kama parokia mwaka 1954, na paroko wa kwanza alikuwa Padre Dino (Joseph Bargetto). Tangu wakati ule hadi leo wamissionari wengi wamefanya kazi ya kitume Parokiani Makambako, kila mmoja akishiriki katika kazi hiyo kadiri ya vipawa vyake ili kuwapelekea watu Habari Njema ya Wokovu na kuwaletea faraja ya kweli. Tunapowakumbuka wenzetu wamissionari hapa tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kazi na mema waliyotenda na haswa kwa ushuhuda wao, vile vile kwa kuwepo wa shirika letu la wamissionari wa Consolata. Hatimaye hata sisi ambao tunaendeleza kazi ya Mungu waliyoifanya tunapata nguvu na ari na hamasa ya fuata nyayo za hawa wazee wetu na washuja wa missioni.
2. Makambako kama mji ina watu 126.415 kutona na sensa ya mwisho ya serekali iliyofanyika mwaka jana mwezi augusti 2023.
3. Jina rasma La parokia hii: Parokia ya Bikira Maria Mama wa Neema.

4. Vigango: 9 mbali na vigango hivyo 9 kuna kingango kimoja tunashikilia au kuhudhumia lakini ni kigango cha parokia jirani ya Ilangamoto watakichua hivi karibuni ako kwenye mikakati ya kutafuta Katekista. Kuna pia kigango kingine kina jengwa huko mta wa Uhuru hatujaanza kusali mahali hapo. Ya kigango tarajiwa cha kibedange Mt. Gabriel wameshaanza kupata hudhuma ya misa na zingine.
5. Jumuiya Ndogo ndogo ya Kikristu: 79

MISSION GALLERY